Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (56), aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kuomba rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba.
Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa jana alimuachia huru Ndassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji chini ya kifungu cha 98(a) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), baada ya Wakili wa Serikali, Denis Lekayo kueleza hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Awali, Ndassa alisomewa mashtaka na wakili Lekayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru ambaye kwa sasa amehama Mahakama hiyo akidaiwa alitenda kosa hilo Machi 13, jijini Dar es Salaam.
#Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)