Mahakama moja mjini Munich nchini Ujerumani imefungua kesi dhidi ya muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa kuchochea hisia za chuki.
Mark Zuckerberg |
Muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg
Jarida la habari la Ujerumani Der Spiegel limeripoti kuwa kesi hiyo iliwasilishwa na wakili mmoja wa mjini Würzburg, anayeutuhumu mtandao wa Facebook kwa kuruhusu wito wa mauaji, vitisho vya machafuko, kukanusha mauaji ya Wayahudi, miongoni mwa mambo mengine.
Sheria zinazodhibiti maneno ya chuki nchini Ujerumani ni kali, ambapo ishara za Kinazi na propaganda za kibaguzi zimepigwa marufuku kabisa.
Mtandao huo wa kijamii umekuwa ukishutumiwa mara kwa mara kwa kuchukua muda mrefu kuondoa habari zenye maudhui yanayokiuka sheria kutoka kwa tovuti yake.