Pamoja na kufanya Muziki, Baby Madaha ana kampuni ya madini

Baby Madaha si wa mchezo mchezo. Wakati ambapo unaendelea kutomsikia kwenye muziki wala kumuona kwenye filamu, usidhani amekaa tu akila bata – anafanya madili makubwa makubwa.


“Mbali na muziki na filamu nina biashara nyingine. Mimi nina kampuni ya madini ambayo ni one of the shareholders inaitwa Afrodium,” ameiambia Bongo5.
“Most of the time nakuwa niko Dubai sababu kwasababu imebase Dubai, UK, Venezuela na Kongo kwahiyo most of the time nakuwa niko kule kwasababu huwezi kutegemea fani moja. Kuna siku nitaacha muziki, sauti yangu haitatoka vile inavyotakiwa au nitabadilisha aina ya muziki, siwezi kuimba Bongo Flava all the time.”
Hata hivyo Baby amesema atakuja na kazi mpya ya muziki na filamu hivi karibuni.