ARUSHA Wakili wa CHADEMA, John Malya amesema wamefungua kesi mahakama kuu kutaka Mbunge Godbless Lema afikishwe mahakamani baada ya kuwekwa mahabusu kwa siku sita.polisi wasema mahojiano hayajakamilika.
Wakili huyo amedai kuwa mtuhumiwa anapaswa kukaa masaa 24 tu kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai. Hivyo kesi imeadhimia kuwataka RCO, Mwenasheria Mkuu na IGP wamlete Lema Mahakamani kwa amri ya Mahakama.
Aidha kwa upande wa Jeshi la Polisi limeeleza kuwa upelelezi juu ya Mbunge huyo wa Arusha Mjini bado haujakamilika.
#Maoni ya Wadau == Wamekataa kumpeleka mahakamani. Wamekataa pia kuruhusu mtu yeyote kumuona. Wamemzuia mkewe kumuona. Wamekataa pia asiwasiliane na Wakili wake. Maelezo ya awali ni kwamba hayo ni maagizo kutoka "juu". Huu ni ukiukwaji mkubwa wa utawala wa sheria. Sheria inasema mtuhumiwa anapaswa kupelekwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 baada ya kukamatwa. However mtuhumiwa yeyote hata awe wa mauaji ana haki ya kuwasiliana na wakili wake. Sasa kwanini Lema azuiwe?? Kuna mambo yanatia hasira sana nchi hii. Halafu bila aibu mtu anasimama hadharani na kusema "Mniombee". #Unafiki.!!