MSANII MKONGWE WA MUZIKI, MR NICE AMESIKITISHWA NA WATU AMBAO WAMEMZUSHIA KIFO KATIKA MTANDAO WA KIJAMII



Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.



Mr Nice ambaye yupo nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigiwa simu kwa nyingi na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuna mtandao umeandika taarifa za uongo kwamba amefariki.

Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:

East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua …kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi.