22 WAKAMATWA KWA UPORAJI WA KUTUMIA SILAHA



Jeshi la Polisi linawashikilia jumla ya watu 22 kwa tuhuma za kuhusika na uporaji wa kutumia silaha kwenye magari na mitaani.

Kamishana wa Polisi, Simon Sirro


Kamishana wa Polisi, Simon Sirro amesema watuhumiwa hao walio na umri kati ya miaka 18 na 19 wamekuwa wakijikusanya katika vikundi na kufanya matukio ya uporaji.

Aidha Kamishna Sirro amesema kuwa jeshi la polisi limewakamata watu wanne wanaotuhumiwa kwa wizi wa magari.