ALICHOSEMA Ben Paul KWA WANAUME WANAOKATAA MIMBA

#BenPol amewataka wanaume kutokutaa mimba kwa sababu kufanya hivyo wanasababisha vifo vya watoto wasio na hatia.

Benpol alidai wasichana wengi wanatoa mimba kutokana na kukataliwa na wanaume wanaowapa mimba hizo.

Benpol👉 “Kuitwa baba ni raha sana jamani watoto ni sehemu kubwa ya faraja, mimi kila siku najiona mpya, lakini kitendo cha wanaume wenzangu kuwapa mimba wanawake na kuwakataa ni kitendo cha aibu na cha kishamba,”

Alizungumza na Gazeti la Mtanzania wiki hii, Aliongeza kuwa angependa kuwaona wanaume wenzake wakijali familia zao ili wasisababishe vifo vya watoto wasiokuwa na hatia.