Stamina amesema alikuwa chimbo kwa ajili ya kuandaa albamu yake mpya

#Stamina amesema alikuwa chimbo kwa ajili ya kuandaa albamu yake mpya ambayo itatoka ndani ya mwaka huu. Rappa huyo ambaye mwaka 2016 alifanya vizuri sokoni kwa kuuza albamu yake ‘Mt Uluguru’ nakala 9,000 na kupata tsh milioni 45, amesema kuwa albamu ni biashara nzuri ambayo wasanii wengi hawajaishtukia.

#Stamina👉“Kweli nilikuwa kimya sana lakini yote hayo yalisababishwa na maandalizi ya albamu yangu mpya,” alisema Stamina. Namshukuru mungu imekamilika na mashabiki mnaweza kukaa mkao wa kula kwa ajili ya albamu mpya,”ameiambia Bongo5

Aliongeza👉“Pia habari njema kwa mashabiki wangu ni ujio wa wimbo mpya hivi karibuni, nimeangalia game ikoje na mimi nikajipanga kwa ajili ya kauenda nalo sawa na kama kawaida yangu huwaga sipotezi. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna mambo mazuri yanakuja,” . .

Alisema wimbo wake huyo mpya ambao yuko mbioni kuuachia tayari ameshashoot na video ili kuhakikisha mashabiki wake wanapata audio na video kwa pamoja🙌 .