UTAACHA KIPI CHA TOFAUTI ILI TUKUKUMBUKE DAIMA?

Nimekaa leo nikaamua nijiulize hili swali; NIFANYE NINI CHA TOFAUTI WAKATI BADO NIPO HAI LEO ILI HATA NIKIFA KESHO KUWE KUNA KITU AMBACHO WATASEMA TUTABAKI KUMKUMBUKA NOEL KWA KUWA ALIWAI KUFANYA KITU FULANI.



Embu nawe nikuulize Unafanya nini ambacho hata kesho ukifa tutabaki kukukumbuka daima?
Steve Jobs atakumbukwa daima kwa kuwa Kampuni ya Apple ipo hapa ilipo leo kwa nguvu na jitihada zake.

What Legacy will you leave behind once you die tomorrow?

Kuacha kumbukumbu si kwamba lazima uwe tajiri sana. Unaweza ukafanya kitu kidogo tu kitakachobadili Maisha ya watu waliokuzunguka mtaani kwako, kwenye jamii yako au kijijini kwenu na ukawa umeacha Legacy ambayo watabaki kukukumbuka kila siku.

Unaweza ukawa ni mtu mwenye mawazo chanya na fikra za tofauti ambazo kama utakuwa unatumia kuleta mabadiliko katika jamii inayokuzunguka ukabaki kuwa ni mtu ambae utakumbukwa daima. Vitendo utakavyovifanya kama ni vizuri, vyenye tija na ambavyo vitaigusa jamii na kuleta mabadiliko chanya vinaweza kukufanya ukumbukwe daima.

Kila sekunde, dakika au saa moja unafanya nini ambacho kitaleta mabadiliko kwenye jamii tu iliyokuzunguka?
Ukiwa maarufu kwa umbea utaishiwa kukumbukwa kwa umbea na majungu uliyokuwa ukiyapiga ila watakaokulumbuka watakuwa ni wachache, tofauti na yule mtu ambae alikuwa akiwaimiza mtaani kwao kuwa wajitahidi kutunza mazingira kwani afya bora ni jambo zuri.

Kuna vingi vya kufanya kwenye jamii iliyokuzunguka ambavyo vinaweza kukufanya watu wakukumbuke daima.
Sio lazima uwe na biashara ndio uweze kumshauri jirani yako ambae unaona biashara yake inasuasua wakati uwezo wa kuinusuru biashara yake ife upo. Mshauri ili kesho biashara yake ikikua akukumbuke daima kuwa ulimnusuru kuifunga biashara yake.

Kaa chini kisha fikiria, je nikifa kesho nitakuwa nimeacha nini ambacho watu watabaki wakinikumnuka? Wafanye wakukubali hata kabla hujafa.

Kumbuka hata uwe na mawazo gani mazuri ukishakufa kabla hujayafanyia kazi hayatokuwa na thamani tena, kwa hiyo yatendee kazi sasa ili kesho ubaki umeacha historia ya kukumbukwa.

Mwandishi: Noel
Instagram: @erinoebusinessconsultancy