NAY WA MITEGO: Bongo Fleva wasiposimama Kidete Kuupigania Muziki wao, Utapotezwa na Siasa

#NaywaMitego amedai kuwa kama wasanii wa Bongo Flava wasiposimama kidete kuupigania muziki wao, kuna hatari ukapotezwa na siasa. Amedai kuwa siku za hivi karibuni mashabiki wamekuwa wakifuatilia zaidi mambo ya siasa kuliko wanavyofuatilia muziki, na anasema hiyo ni hatari.

#NaywaMitego👉 “Watu walikuwa wanasikiliza siasa zaidi kwamba leo nini kinaendelea, leo kiongozi gani ameongea kitu fulani, nafikiri sasa ni time ya sisi kupambana kuurudisha muziki wetu kwenye line, kuurudisha muziki wetu watu wausikilize muziki, siasa na vitu vingine ambavyo vinaendelea, skendo, kiki, viwe vya baadaye,” alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ. Pia ameonya kuwa kama wasanii wa muziki wasipokomaa, wanaweza kujikuta wakipumulia mashine kama wenzao wa bongo movie ambao soko lao linazidi kuporomoka.

Kwa upande mwingine amedai kuwa wimbo wake Wapo umefanya muziki uanze kusikilizwa tena. Ijumaa hii rapper huyo anakutana na Rais Dkt John Magufuli baada ya kuitwa Ikulu kufuatia wimbo wake Wapo uliokosoa serikali. . .