Alichosema MkubwaFella kuhusu Kurudi kwa kundi la YAMOTO BAND

#MkubwaFella afunguka kuhusu #YamotoBand Na  kusema kuwa sababu iliyosababisha #yamotoband kuwa kimya kwa kipindi chote ukamilishaji wa tathmini itakayojumuisha kazi waliyoifanya kwa kipindi chote na kupanga uimara wa mipango ya kwenda mbele zaidi.

#MkubwaFella👉 “Sio kila siku kwamba utatoa ngoma, umetoa ngoma haya tafutia hela ya zile ngoma ulizozitoa na kikubwa mwanzo mwanzo unatafuta ukubwa ukishapata ukubwa unaanza kutoa ngoma taratibu taratibu sio kila siku, kila wiki kila mwezi unatoa ngoma unashindana na nani?, uzuri yamoto wamezaliwa kwa mtu anaejua mziki na ndo meneja wakwanza kwahiyo siasa zote za muziki nazijua kwahiyo lazima tupange mipango ya kwenda  na kuangalia mashabiki kama tunao”Aliiambia dizzm online . . #socialmediahabari