JayMoe aeleza jinsi alivyopata aibu baada ya kumdharau #Billnass

#JayMoe amefunguka licha ya kutamani kufanyakazi na #Billnass lakini hatasahau alivyomdharau kabla ya kusikiliza na kuona video zake. amedai kabla ya kumwona, kusikiliza na kutazama video zake hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alipotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake alidharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini. #Jaymoe👉

“Unajua kuna siku meneja wake, Bill Nas ‘Mchafu’, alinitumia wimbo akiniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo, nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wapo kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania,” aliliambia Gazeti la Mtanzania.

Aliongeza👉“Hapo nikajifunza kitu kuwa hutakiwi kumdharau mtu, maana dogo ana uwezo mkubwa wa kurap na anajua nini anafanya hadi nimemwahidi kufanya naye kazi,” . Alimalizia kwa kusema licha ya kutamani kufanya naye kazi pia anatamani kumtungia mashairi #Billnass kama atakuwa tayari. . .