Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo inatarajia kupambana na timu ya taifa ya Ghana chini ya miaka 17 Black Starlets kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Uwanja wa Taifa,
Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa kumi jioni utatumika kama ishara ya kuwaaga watanzania kabla ya kusafiri kwenda fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana nchini Gabon yanayotarajiwa kuanza Mei 14, mwaka huu.
Kabla ya kutua Gabon,Serengeti Boys itakwenda Rabat, Morocco kufanya kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5, Ikiwa huko itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji Morocco na timu nyingine ya jirani kati ya Tunisia au Misri.
Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri kwenye soka la vijana