Linah adai Wazazi wake walimkataa mpenzi wake aliyempatia Ujauzito

#Linah adai wazazi wake walimkataa mpenzi wake aliyempatia ujauzito Msanii wa muziki #LinahSanga ambaye kwa sasa ni mjamzito amefunguka kwa kudai kuwa wazazi wake walimkataa mpenzi wake wa sasa kwa kigezo cha dini.

Muimbaji huyo ambaye amelelewa katika misingi ya dini ya kikristo, amesema kuwa haikuwa rahisi kwa wazazi wake kumkubali mwanaume huyo. #Linah👉“Mwanzoni wazazi wangu walimkataa mpenzi wangu kisa ni dini tofauti na mimi, lakini sasa hawana pingamizi,” alisema Linah.

“Tumeunganisha damu na kwenye mahusiano naamini upendo, nisingependa mtu anipangie, lakini jambo la wazazi kwa familia za kiafrika ni tofauti,”alizungumza hayo kwenye XXL Clouds

Aliongeza👉“Nimebeba ujauzito katika right time kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa kabisa muda wowote.”