Majina ya Wabunge Afrika Mashariki waliochaguliwa

Jana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura kuchagua wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.

Baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa kuiwakilisha nchini.

Tanzania inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana yalitangaza washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura nyingi za hapana, na hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.

Kati ya wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama cha Wananchi (CUF). Wagombea wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za hapana. Fancy Nkuhi (CCM) Happiness Legiko (CCM) Maryam Ussi Yahya (CCM) Dkt Abdullah Makame (CCM) Dkt Ngwaru Maghembe (CCM) Alhaj Adam Kimbisa (CCM) Habib Mnyaa (CUF)