Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama hicho kitaendelea kufanya mambo kiungwana kwa kuwa Tanzania ni nchi ya amani na kuwa hakuna CUF ya Maalim Seif wala CUF ya Lipumba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Maalim Seif alisema CUF inatimiza wajibu wa kutunza amani na iwapo kingetaka kuleta machafuko basi kingefanya hivyo tangu zamani.
“CUF ni moja. Ni kweli sisi tumekuwa wapole na waungwana, sisi si tunaambiwa hii nchi ya amani, sisi tunatimiza wajibu wetu wa kutunza amani. Hakuna chama kinachotunza amani kama CUF” alijibu mara baada ya kuulizwa na waandishi wa habari.
“The struggle we continue, mtatia ndani Maalim Seif, mtatia ndani Mtatiro lakini there are so many Maalim Seif’s. Kuna Maalim wengine ni vichaa,” alisema
Wakati huhuo Maalim Seif aionyooshea kidole Rita
Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad amezungumza na waandishi wa habari leo na kusema Wakala wa Usajili wa vizazi na vifo, (RITA) utakuwa umekiuka sheria iwapo utaisajili na kuitambua bodi ya wadhamini iliyoundwa na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba.
“Sisi tumekuwa wapole sana, tunaona katiba inavunjwa, lakini niseme kwamba, kama Rita wataisajili bodi ya Lipumba, watakuwa wamekiuka sheria yao wenyewe. Bodi ipo na imesajiliwa 1993 na tunacho cheti cha kusajiliwa” alisema
Alisema ni utaratibu kuwa kila kipindi fulani marekebisho hufanywa lakini bodi haifi.
Alisema bodi ya CUF ipo na kama ofisa Mtendaji mkuu wa Rita ataisajili basi ajue anavunja sheria.
D