MAMA SALMA AAPISHWA RASMI LEO BUNGENI


Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai leo amemuapisha mke wa rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Rashid Kikwete kuwa mbunge wa Bunge wa kuteuliwa.

Mh.Salma aliandamana na mumewe rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye uwepo wake ulisababisha kelele za shamra shamra kutoka kwa wabunge wakisema kwa sauti 'tumekumiss tumekumiss'.

Mkutano wa saba wa bunge la umeanza kikao chake cha kwanza cha mkutano wa bajeti hii leo.