HARMORAPA ASHAMBULIWA STEJINI

Meneja wa msanii anayefanya vizuri kwa sasa Harmorapa, Iren Sabuka amesema kuwa rapper huyo almanusula aumizwe wakati anaperforme kwenye ukumbi wa Maisha Club siku ya Jumamosi
Sabuka amesema kuwa Harmorapa alirushiwa chupa na shabiki mmoja wakati anaperform lakini kwa bahati mzuri aliikwepa hivyo hakuumia wala kupata madhara yoyote

“Kiukweli hili jambo la kusikitisha sana, Harmorapa alikuwa stejini ana perfom ila kabla ya kumaliza show alitokea mtu mmoja akarusha chupa stejini bahati nzuri Harmorapa alikwepa ile chupa. Laiti asingekwepa au ingemkuta kwa bahati mbaya sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine,” amesema meneja huyo.

Aidha Meneja huyo aliongeza kuwa ameshangazwa na kusikitishwa mmono na kitendo kilichofanywa na shabiki huyo kwakua si cha kiungwana hata kidogo ukizingatia hamorapa bado anatafuta kama wataftaji wengine

“Mimi naona kile kitendo ni wivu tu sababu watu hawajui maisha kila mtu ana namna yake anayotokea. Harmorapa ametokea mtaani anatafuta maisha yake leo anaibuka mtu anamrushia chupa na kutaka kumjeruhi, anaibuka mtu mwingine anasema kuwa anataka kumuonesha na kukomesha,”