Mh Temba aelezea Mfumo wa Utoaji Nyimbo #TMK

#MhTemba afunguka kuwa hapo zamani kundi la #TMKWanaumeFamily lilikuwa haliachii kazi za wasanii wao kwa nafasi bali walikuwa wanampatia nafasi msanii yeyote aliyekuwa anakubalika katika kipindi husika.

#Temba alikiambia kipindi cha On The Eight cha ETV, msanii yoyote ambaye wimbo wake umepokelewa vizuri basi atapewa nafasi zaidi kwa kipindi hicho hata kwa kuachia albamu ili kuwafurahisha zaidi mashabiki wao.

#Temba aliongeza kuwa hata wazo la kuanzisha kituo cha Mkubwa na Wanawe lilianzia kwake kutokana na matatizo kadhaa yaliyowahi kujitokeza huko nyuma kwa baadhi ya wasanii wenzao kujitoa kwenye kundi kwa madai walikuwa wanadhulumiwa na #SaidFella..