TID amefunguka, Support imepungua baada ya Kuacha

#TID amefunguka na kusema sasa hivi watu ambao mwanzo walikuwa wakimpa support kwenye muziki na mambo yake mengine wamemtosa na hawampi msaada wowote hivyo kila kitu anapambana mwenyewe.

#TID amedai watu hao wameacha kumpa suport baada ya yeye kuachana na madawa ya kulevya hivyo saizi wao wanamuona yeye ni kama msaliti.

#TID👉 “Saizi kila kitu nafanya mwenyewe hata hao mabrother unaosema washanitosa maana wao walikuwa wanapenda kuona nazidi kuharibika, hivyo toka nimetangaza kuachana na madawa ya kulevya wao wananiona mimi kama ‘snitch’.ameiambia Planet Bongo Alhamisi hii TID . .

Aliongeza👉“lakini hilo halina tatizo kwani mimi mwenyewe niko vizuri ndiyo maana unaweza kuona video hii nimetumia pesa nyingi kuifanya na nimelipa mwenyewe, hii pesa ningesema ninue gari basi ningepata Mark X nyingine lakini nimeamua kuiweka kwenye video ili kuleta ubora zaidi”. . . #TID leo ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Woman’.