Mourinho:Hakuna furaha zaidi ya kuwafunga chelsea


Baada ya kufanikiwa kuifinga timu yake ya zamani ya Chelsea goli 2- 0, katika uwanja wa Old Traford, Meneja wa Timu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa kitendo hicho ni furaha kubwa sana kwake na kwa timu yake kwa jumla

Jose Mourinho ambaye aliifundisha Chelsea kabla ya kujiunga na Manchester United mwanzoni mwa msimu huu amefanikiwa kuifinga timu hiyo kwa mara ya kwanza akiwa kama boss wa United

"Sina furaha nyigine zaidi ya kuifunga Chelsea - tumewafunga vinara. Haijalishi kama kinara wa msimamo wa ligi ni Chelsea au ni timu nyingine, lakini tumewafunga bila utata. Hakuna yeyote anayeweza kutilia shaka ushindi wetu