Aliko Dangote amesema ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal

Tajiri namba moja barani Afrika, Mnigeria, Aliko Dangote amesema ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal ya England katika kipindi cha miaka 4 ijayo. Dangote mwenye utajiri wa £8.3 billion alishawahi kutaka kununua hisa katika klabu hiyo lakini ilishindikana, Arsenal inakadiriwa kuwa na thamani isiyopungua £1 billion.