Barakahtheprince akanusha kuhusu Picha na Video ambazo zinasambaa Mtandaoni

Toka siku ya jana kumekuwa na picha na video ambayo inamuonyesha Barakahtheprince na msichana mwingine wakiwa katika hali ya mahusiano ya kimapenzi.




Kayaandika haya kwenye akaunti yake ya Instagram Kuna video na picha zinasambaa mitandaoni kutoka kwa #Soudbrown kuwa eti kuna binti anaitwa Bety alikuwa mwanamke wangu..kwanza niwatake radhi sana mashabiki wangu, kwa haya mapicha picha ya kila siku nayotengenezewa...huyu binti sio bety na wala sio uyo ambae kahojiwa na #Soudbrown nakumbuka kuna kipindi cha nyuma nilitengenezewa mdogo wangu fake na hao kina soud na alikuwa akiongea vibaya sana katika kipindi cha kwenye tv cha #Soudbrown kuhusu mimi na Najma pia na mama yangu mzazi.. Ambapo sio vitu vya kweli na uyu dogo simfaham kabisa ndio maana sikutaka kufatilia chochote wala kuongelea chochote, hivi mtu unaweza kuacha kumjali mama yako mzazi aliekusomesha na kukubeba tumboni miezi tisa na kuteseka na wewe?? 

Limepita hilo leo linaletwa jipya tena... Huyu binti tulikuwa location tukishoot video ya msanii anaitwa #Brayani Jana maeneo ya #Ramada na hata dir wa video #jouze anaweza kuwa shahidi na hata mke wangu mwenyewe ni shahidi sasa, kumbe huyu akapiga picha na kurecord video pasipo mimi kufahamu nakumtumia #Soudbrown.... Ndugu zangu mashabiki msiamini jambo lolote linaloendelea katika mitandao ya kijamii.. Kuhusu hii video na picha kwasababu ushahidi upo... muda mwingine kuna mawakala wa kutuchafua na kuchafua sifa zetu wanatumwa kutuchafua... Na kwa hili nataka nimfurahishe safari hii, Hatua za kisheria zitachukua mkondo wake... Nawapenda sana na niwaombe radhi kwa kinachoendelea mitandaoni..

#IamRockstar 
#IamPrince 
#RockStar4000