Julius mtatiro ashiriki Mkutano maalum unaoangazia Changamoto za Vyama visivyo madarakani

Kupitia akaunti yake ya Facebook Julius Mtatiro ambaye anaongoza kamati ya uongozi wa Cuf yupo Afrika kusini akishiriki mkutano wa vyama ambavyo havipo madarakani na kungalia changamoto zake.



Kaandika haya katika akaunti yake ya Facebook Nashiriki mkutano maalum unaoangazia Changamoto za Vyama visivyo madarakani. Nitawasilisha MADA mbele ya wakuu wengine wa vyama akiwemo #Mmusi_Maimane, kiongozi wa DA ya Afrika Kusini, Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani nchini Zimbabwe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani nchini Zambia, Lesotho n.k. Kutoka Afrika Mashariki, ni CUF pekee ndiyo imepata heshima ya kuwakilisha. Mkutano huu umeandaliwa na FPD na ADI (Mashirika yanayosimamia Demokrasia, Kusini mwa Afrika). Mada ntakayoiwasilisha ntaifasiri baadaye na kuwawekea mtandaoni. Wikendi njema.

Julius Mtatiro,
Johannesburg.