Coaster, DCM zatolewa kama daladala Posta, Kariakoo



Katika kile kinachoonekana kuwa ni utekelezaji wa jitihada mbalimbali za kupunguza foleni maeneo ya katikati ya jiji, magari yote ya abiri yasiyo na uwezo wa kubeba watu 40 yanaendelea kufutwa katika orodha ya magari yanayoruhusiwa kuingia mjini. 

Aidha, hadi kufikia wiki hii, tayari mabasi mapya 531 yanayobeba abiria zaidi ya 40 yamekuwa yakitoa huduma kwenda maeneo hayo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam yakiwamo ya Posta na Kariakoo, ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuyaondoa mabasi madogo.

Aidha, imefahamika kuwa uamuzi huo wa sasa unatarajiwa kuathiri mabasi kadhaa maarufu ya daladala jijini Dar es Salaam yakiwamo ya Toyota Coaster na DCM, ambayo uwezo wake ni kubeba abiria wa idadi chini ya 40.

Akizungumza na Nipashe, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara, Johansen Kahatano, alisema Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imeanzisha utaratibu huo kama namna ya kukabiliana na tatizo la foleni na usumbufu kwa wasafiri. 

#Nipashe