DARASA HURU: MAFANIKIO YA KWELI YANACHUKUA MUDA

Kila Mtu anapenda kufanikiwa Maishani. Na uzuri wa mambo ni kwamba kila mtu ana aina ya Mafanikio anayoyahitaji maishani mwake. Kuna ambae akimiliki Biashara zake na zikawa zinaenda vizuri anajiona kapata mafanikio yote anayoyataka.



Kuna ambae akisoma na kufaulu anajiona amepata mafanikio yale anayoyataka. Kuna ambae akioa au akiolewa anajiona tayari kashapata mafanikio yote anayoyataka. Kila mtu ana namna ambavyo anayachukulia Mafanikio. Lakini kitu kikubwa cha kufahamu ni kuwa hakuna Mafanikio ya haraka.

Mafanikio ya kweli yanachukua muda kuyapata. Mafanikio ya kweli hayaji kwa siku au saa au dakika kadhaa. Hivyo yakupasa uwe mvumilivu. Angalia watu wote ambao leo hii unawaona wamefanikiwa imewachukua miaka na miaka mpaka kupata hayo mafanikio unayowaona nayo.

Hawakulala usiku na kuamka asubuhi wakiwa na mafanikio. Walipitia vikwazo vingi, changamoto nyingi, kufeli kwa wingi, kukatishwa tamaa sana lakini kwa kuwa walitambua wanachokitaka maishani hawakuvunjika moyo walizidi kusonga mbele na ndio maana leo hii tunasema wamefanikiwa.

Waliofanikiwa wanaendelea kuwa wachache kwa kuwa kawaida ni watu wachache ambao wana moyo wa kuvumilia, kusema ngoja niendelee kusubiri ili nipate mafanikio ninayoyataka.

Kumbuka hata ukitaka mtoto huwezi ukalala tu na mwanamke leo na kesho akaamka kajifungua, itachukua muda. Na hivyo ndivyo ambavyo pia Mafanikio yalivyo. Mafanikio ya kweli ni kwamba UNAKUBALI KUPANDA MBEGU BORA LEO, ili kusudi UJE KUVUNA SIKU ZA MBELENI.

#BeInspired #BeMotivated #StayHungry #BePositive #DoNotGiveUp #DoNotQuit #SelfEntrepreneur #SelfMadeEntrepereneur #SuccessMindset #Successful #RealSuccessTakesTime 

Inspired by Noel.
INSTAGRAM @noellove100