Diamond kuungana na Ne-Yo kwenye ziara ya Uingereza, Disemba

Diamond Platnumz na Ne-Yo wameunganisha nguvu ya pamoja kuishambulia Uingereza. Wawili hao watakuwa na ziara ya pamoja mwezi Disemba mwaka huu.




Taarifa hiyo imetolewa kupitia akaunti ya Instagram ya Revolt Africa. "Africa & America join forces!! @DiamondPlatnumz & @Neyo UK tour this December! The movement continues... #AfricaToTheWorld #MusicToTheWorld #Neyo #neyonation #diamondplatnumz #rnbking #rnb #Tanzania #africa #afropop #afrornb #afrobeatsuk #afrobeats #afrobeat #kidogo #wcb #revolttvafrica #afroBeHeard," wameandika.

Wakali hao wenye wimbo wa pamoja uitwao Marry You, watafanya show sita kwenye majiji mbalimbali nchini humo. Mara ya kwanza Diamond aliongelea ujio wa ziara yao kupitia mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita.

Anadai kuwa katika kipindi cha hivi karibuni Ne-Yo amekuwa mshkaji wake wa karibu. "Tumekuwa tuko close sana na Ne-Yo, tunawasiliana mara kwa mara na of course vitu vingi namuuliza na najifunza kupitia kwake," alisema. "Ukiangalia hata kwenye clip moja wakati nashoot video kuna mapande yake fulani alikuwa anayapiga mimi nilikuwa namchungulia kwa mbali 'kwamba unafanyaje wewe.' Mimi kila ninayeshuti naye video namkalisha lakini bro [Ne-Yo] alikuwa ananifanya kitu mbaya, nilikuwa namzoom namuangalia 'hivi unafanyaje' nikampa na mimi mapande yangu ya uongo na kwali," aliongeza. "Ni mtu ambaye inawezekana Disemba tukawa tuna project kubwa sana."

BONGO 5