Prof.Kitila na Zitto wamelikwepa swali la kitoto kabisa.Afande anapaswa kujibiwa in SOCIAL MEDIA si OFFICIALY.
Zitto kabwe na Prof.Kitila Mkumbo wamebaha jipu limewapasukia usoni likatiririkia machoni sasa maji yake yanawasha wameshindwa kujikuna wakijikunia hadharani watu wataona na wata-aibika.
Ni siku Tatu sasa imepita tangu Simba wa pori Afande sele The King(Sulemani Mshindi) alipowakurupua viongozi wake mafichoni walipokuwa wamejifichia wakirusha mashambulizi dhidi ya Upinzani wa kweli UKAWA,wao walidhani watakuwa accepted kwa maovu wayafanyayo.
Sulemani Mshindi baada ya kueleza malalamiko yake mengi lakini hoja kubwa hilikuwa ni swali Je ninyi viongozi wangu (Zitto na kitila)Ninyi ni Malaika au Shetani akaongezea akasema je ninyi ni Baridi au Moto ni heri muwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu....maana maandiko yanakataza kuwa vuguvugu (yaani mtu husiye eleweka,kigeugeu,ndumila kuwili.
Majibu ya Zitto Kabwe alijikanyaga kwa aibu na kujikanyaga lakini alifikia hitimisho bila kujibu kuwa wao ni Malaika au Shetani-Moto au baridi? Zitto alichokisema nikuwa malalamiko ya Afande Sele #Watayafanyia_kazi mara o wanachama hawakupendezwa na kuhoji kwa Afande sele,mara ni haki yake kikatiba kuhoji.
Sasa swala eti watalifanyia kazi ni kazi hipi hiyo ambayo inaenda kuanywa je nikumuonya Afande Sele hasitoe siri za viongizi wa chama au ni kazi gani hiyo inayoenda kufanyika?.Kama atajibiwa Official Afande Sele atakuwa hajatendewa haki maana Afande amehoji kwenye Social media na kama angeona malalamiko yake yangefaha kuwa in Official letter basi angefanya hivyo lakini hakuona umuhimu wa kufanya hivyo kwani Chama kinajipambanua kuwa ni #Transparence and #Uzalendo sasa ukifatilia kwa umakini ni kwamba kati ya Afande na viongozi wake Mwenye Transaraence na Uzalendo ni Afande kwani ndiye aliyetekeleza msingi mkuu wa ACT wazalendo.
Majibu ya Zitto Kabwe yalipaswa kujibiwa kwenye Social Media si mafichoni na majibu yalikuwa simple ni kujibu tu kuwa sisi ni Malaika au Shetani-Moto au Baridi full stop si kuzunguka zunguka mara 'o' tunamuheshimu inamaana hapo hawali walikuwa hawamuheshimu? au mpaka makaburi yafukuriwe ndio mtangaze idadi ya watu wanaowaheshimu? mara 'o' wanachama hawajafurahishwa.Hili siyo Jibu
Majibu ya Prof.Kitila Mkumbo naye alimjibu kama bosi wake alivyomjibu kimagumashi eti anasema tunamheshimu Afande Sele Eti ametumia haki yake kikatiba msingi namba kumi inayompa mwanachama haki ya kutoa maoni,Kitila anachanganya Afande akutoa maoni alitoa tuhuma na alihitaji majibu kwa njia aliyotumia kutolea tuhuma hizo..Kumjibu Official ni kumyima haki yake kikatiba kama wanavyojipambanua wazee wa UWAZI NA UWAJIBIKAJI kama kweli wanaenenda hivyo kwanini wanakwepa kumjibu Afande in social media wanakimbilia kumjibu OFFICIALY?This is not Fair.(Reference) kipindi Bwana Fred Mpendazoe alipotoa tuhuma kwa cha kupitia mtandao wa kijamii Mh.Tundu Lissu alimjibu kwa account yake ya FB kwa majibu sahihi kulingana na tuhuma alizotoa wala hawakusema tutalufanyia kazi kwani swali lake halikuwa siri lilikuwa wazi ana lilijibiwa very Openly.
Prof.Mzima na msomi wa mambo ya uchumi(zitto) wamepoteana kwenye kaswali ka kawaida sana huku wakipoteza lengo kwa kusingizia eti "INGELIKUWA VYAMA VINGINE VINGEMFUKUZA.So what? je hilo ndilo jibu? What is the hell?. Kama Mmeanzisha chama chenye wanachama malaki na mmeulizwa swali na mwanachama mmoja kati ya malaki ambao wameficha maovu yenu mmechanganyikiwa,mmebaha sasa je wakiuliza hata watano si mtaikimbia ofisi?
Hahahahaha....ACT -Wazalendo Leo na Kesho.Bahati mbaya sana kesho yenu ninyi na viongozi wenu hamuijui.
Emanuel J John