Fiesta ya Dar: Yemi Alade, Chameleone na Tekno kutumbuiza

Fiesta 2016


Yemi Alade alishinda tuzo ya msanii bora wa kike, na Tekno akachukua ya msanii bora aliyechipukia kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 – hawa wawili hawakwepeki na hakuna ubishi ni miongoni mwa wasanii wa moto zaidi Afrika kwa sasa.

Wapopo hao wametajwa kutumbuiza kwenye kilele cha tamasha la Fiesta, litakalofanyika jijini Dar kwenye viwanja vya Leaders, November 5.
Hiyo sio mara ya kwanza wawili hao kuja Dar. Supastaa na nguli wa muziki wa Uganda, Jose Chameleone naye atatumbuiza kwenye show hiyo.
Wasanii wengine watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Alikiba, Raymond, Mr Blue, Belle 9 ba wengine. Bado haijajulikana ni msanii yupi kutoka Marekani atakayetumbuiza mwaka huu.
Chanzo: Bongo5