Diamondplatnum na Wema Sepetu wapatana na kuwashangaza Mashabiki wao



Baada ya wasanii hawa wawili kuvunjika kwa mahusiano yao kwa zaidi ya Mwaka mmoja sasa kulikuwa na kutokuelewana na kupelekea ugomvi kuwa mkubwa zaidi kwa mashabiki zao. Na kupelekea kuwa team Diamond na Team wema hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Miezi ya hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio yaliyoashiria kurudi kwa maelewano baina ya wasanii hawa wenye mashabiki wengi katika tasnia sanaa. Baadhi ya matukio na pale Wema Sepetu alipomuombea kura Diamond kupitia kurasa yake ya Instagram. Na tukio jingine ni pale Diamond alipo post tangazo la tamasha aliloandaa Wema Sepetu.

Hata Diamond alipohojiwa na Soudbrown kupitia CloudTv alikili kuwa hawana Ugomvi na Wema ila Baadhi ya mashabiki wanakuza mambo na akaongezea kuwa Mama watoto wake Zari ana tatizo lolote na mpenzi wa zamaniwa Diamond yoyote yule.

Na tukio la hivi karibuni limewashangaza zaidi mashabiki ambao wanachochea Bifu hilo ni pale Diamond alipo Muwish Wema Sepetu katika siku yake ya kuzaliwa. Na siku ya jana Wema pia amemuwish Diamond katika Siku yake ya kuzaliwa.

Maneno ya Wema na akaposti picha hiyo hapo chini
Help me to wish major happy birthday to my libra mates... @ecejay @counsellorsalaah @diamondplatnumz @mcpilipili 


Maneno ya Diamond na akaposti picha hiyo hapo chini 

Help me to wish major happy Birthday to all my LibraMates @chokadj @maulidwadi @wemasepetu @agatonny