Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuanzishwa mfumo mpya wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki.



Hatua hiyo ina lengo la kurahisisha upatikanaji wa mapato halali ya serikali pamoja na kuwafanya madereva na makondakta, kuajiriwa rasmi na wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri. Pia mamlaka hiyo imezindua kampeni ya usafi kwa wafanyakazi wa daladala, ambayo inawataka kubadilisha sare za madereva na makondata, ambazo walishonewa na matajiri wao.

Sasa wafanyakazi hao watashona sare zao wao wenyewe ili wawe na uhalali wa kuzimiliki na kuzifanyia usafiri wa mara kwa mara. Mkurugenzi wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano alisema jana kuwa mfumo huo wa tiketi za daladala kwa njia ya elektroniki, utaanza kutumika Januari mwaka kesho.
Lakini, aliongeza kuwa kuanzia Desemba mwaka huu, watafanya mpango huo kwa majaribio kwa mabasi yaendayo mikoani. #HabariLeo