Maneno ya Serikali Baada ya kusambaa Video ya Mwanafunzi kufanyiwa Vitendo vya Kikatili



Waziri wa Wizara ya TAMISEMI, ameagiza kushushwa cheo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbeya Day. Inadaiwa Mwalimu Mkuu huyo alitaka kuficha tukio la kupigwa kikatili kwa Mwanafunzi.



Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amewafukuza chuo Waalimu waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo Shule ya Mbeya Sekondari kwa kumpiga kikatili Mwanafunzi. 
Sakata hili limeibuliwa na picha ya video iliyokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii.