Maoni ya Malisa GJ Baada ya Kauli ya Serikali kulaani kitendo alichofanyiwa Mwanafunzi wa sekondari Mbeya



Huko Mbeya kuna wanafunzi wa chuo wamemchangia mwanafunzi mwenzao wa sekondari na kumpiga, mawaziri watatu wametoa tamko rasmi juu ya tukio hilo. Alianza Mwigulu Nchemba, kisha Prof.Ndalichako na leo Mhe.Simbachawene. Wote wanalaani vikali kitendo hicho na kutoa rai vyombo vya dola vichukue hatua. Wao kama mawaziri wamechukua hatua pia ikiwa ni pamoja na kuwafukuza vyuo wanafunzi hao wa ualimu.

Lakini najiuliza kuna wanafunzi wangapi Tanzania wanaopigwa, kuteswa na kunyanyaswa na waalimu wao zaidi ya huyo wa Mbeya lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa sababu tu hawakurekodiwa video? Kwanini mawaziri wasideal na mfumo badala ya tukio moja moja? Je wengine wanaopigwa na kudhalilishwa huko Mbinga, Newala, Igunga, Rorya etc waendelee kupigwa kwa sababu hakuna mtu wa kuwachukua video na kuonesha impact ya wanayofanyiwa?

Anyway, yule jamaa aliyekua anapiga watu huko Buguruni kwa ubabe tu, na majuzi akamng'oa mtu macho Waziri gani katoa tamko? Waziri mkuu? Waziri kamili? Naibu waziri? Waziri kivuli?? Sometimes we need to be fair.!!

Malisa GJ