Ahadi alizotoa Paul Makonda baada ya Kumpatia Matibabu mgonjwa aliyetobolewa Macho



Nianze kuwashukuru ndugu zangu wa Clouds hasa kipindi cha #LeoTena kwa sauti zao mpaka kumfikia ndugu yetu Said ambaye alitobolewa macho kinyama kwasasa haoni tena. Mh Mkuu wa Mkoa ndugu @paulmakonda 
@dahuuofficial @musahussein Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi Majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu Hataweza kuona tena kwa maisha yake yote. 
Serikali ya Mkoa imejitolea;
 
. Kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena.

-•Kumpatia Elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira.

-•Serikali ya Mkoa imetoa Gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake

-•Vilevile Serikali yetu itatoa kiasi cha Shilingi milioni kumi kama sehemu ya Mtaji kabla ya kupatwa na ulemavu alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwa kuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja.