Maoni ya Zitto Kabwe kuhusu Vurugu baina ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Lema



Siku ya jana katika sherehe ya kuweka Jiwe la msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Akina Mama na Mtoto kulitokea mvutano kati ya Mkuu wa Mkoa na Mbunge wa Arusha mjini na kuzua Taharuki kwa wageni na wafadhili wa mradi huo. Huku Mbunge akilalamika kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha kavuruga ratiba ya Hiyo ya Kuweka jiwe la msingi.

Maneno ya Zitto Kabwe baada ya tukio

Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu  Mrisho Gambo una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. Kaa Na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja.

Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.