Morogoro: Lori lililokuwa likisafirisha nyanya aina ya fuso kugongana na tenka la mafuta na Watu saba wafariki

Watu saba wamefariki dunia papo hapo na mwingine mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya lori lililokuwa likisafirisha nyanya aina ya fuso kugongana na tenka la mafuta katika eneo la Fulwe,Mikese barabara kuu ya Morogoro- Dar-es-Salam ambapo miongoni mwa waliokufa ni madereva wa magari yote mawili.



Ajali hiyo imehusisha lori aina ya fuso lenye namba za usajili T 153 ASC mali ya Felician Kinguza,lililokuwa na shehena ya nyanya,likitokea Msowero wilayani Kilosa,kuelekea jijini Dar es Salaam likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina moja la Patrick,ambalo limegongana na tenka la mafuta aina ya Scania,mali ya Mlay,majira ya saa nane usiku,ambapo inadaiwa fuso lilijaribu kulipita gari dogo aina ya Corola na ghafla dereva alikutana na tenki na kugongana hivyo kusababisha ajali hiyo.

Wananchi hao wameshauri kupangiwa muda maalum kwa malori ya mizigo kutembea barabarani kama ilivyo kwa magari ya abiria,kwani mengi yamekuwa yakilazimishwa na madalali kuwahisha mizigo sokoni,hata dereva anakuwa amechoka.

Afisa Muuguzi Mkuu Msaidizi,Edwin Damas, amekiri kupokea miili ya marehemu hao saba ambayo imeharibika vibaya hivyo kuwa vigumu kutambulika kirahisi,sambamba na majeruhi mmoja mwanaume,ambaye atahamishiwa hospitali ya Muhimbili. Pamoja na taarifa kutoka eneo la tukio kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa lori aina ya fuso,polisi wameshindwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na ajali hiyo.


 ITV