Polisi wapya walilia mishahara miezi minne



WAKATI kasi ya uhakiki wa watumishi hewa ikiendelea, imebainika baadhi ya taasisi za Serikali ikiwamo Jeshi la Polisi halijawalipa mishahara askari wake wapya walioajiriwa Juni, 2016 kwa kipindi cha miezi minne sasa.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo yaNdani ya Nchi, Christina Mwangosi, zinasema askari wapya hawajalipwa mishahara kutokana na maandalizi ya mfumo mpya wa malipo. “Unajua kuna taratibu za malipo zinaendelea kufanyiwa kazi, hivi sasa majina yao yanaingizwa kwenye mfumo wa malipo kutokana na uhakiki unaondelea. “Kuna baadhi yao hawajalipwa, lakini wizara inaendelea kuwaingiza katika mfumo huo, tunaamini watalipwa pindi taratibu zote zitakapokamilika,” alisema Christina.

#Mtanzania