DARASA HURU: SIWEZI KUMUDU



SIWEZI KUMUDU, ni neno dogo na fupi sana lakini lina maana kubwa na endapo utaliheshimu unaweza kufika mbali sana na hata Ku-Achieve Financial Freedom (Uhuru wa Kifedha). Wengi tunafeli maishan hasa vijana na tunashindwa kuwa na uhuru wa kifedha kwa kuwa tunaishi na kufanya matumizi yaliyo juu ya uwezo wetu wa kifedha.

Jiulize una vyanzo vingapi vya mapato?
Unajua inakugharimu kiasi gani kuishi?

Na je unaishi ndani ya uwezo wako? (Do you live within your means?) Jana ilikuwa ni wikiendi naamini katika siku ambazo watu hufanya TOO MUCH UNNECESSARY SPENDINGS NI WIKIENDI.

Wengi tunachanganyikiwa hasa likija swala la kutumia (spending), lakini si kama hatujui tiba ya kuepukana na matumizi mabaya ya pesa ila tu kuna katabia tunaogopa kukionyesha kwa watu wetu na haka katabia kenyewe kanaitwa katabia cha kuogopa kusema SIWEZI KUMUDU (I CAN'T AFFORD IT). Sio kwamba unakuta hujui kuwa hii hela ninayotaka kuitumia sikuipangia bajeti kufanyia hichi ninachotaka kukifanya, au sio kwamba hujui kwamba nikitumia hii hela kesho sijui hata nitaishije lahasha bali tunahofia sana kuwaambia wenzetu hapana leo SIWEZI KUMUDU.

Matokeo yake wenzio wakikupigia simu bwana twende out tukale bata utasema poa ngoja nijiandae tukale bata....lakini swali ni je ulibajetia hiyo hela unayotaka kwenda kuilia bata? Na je utakuwa unaishi ndani ya uwezo wako?

Wengi wetu tuna chanzo kimoja tu cha Mapato aidha AJIRA AU BIASHARA. Jiulize unaingiza kiasi gani kwa mwezi, je ukikibajetia kwa siku mpaka huo mwezi uishe utaweza kutumia na hapo hapo kusevu pamoja na kuwekeza kwenye vitega uchumi vingine?

Kama jibu ni HAPANA usione ugumu kuwaambia rafiki zako kuwa leo SIWEZI KUMUDU gharama za kula bata so I better stay at my home, unavunga sana na kuogopa wenzio watakucheka huku ukisahau kuwa YOU ARE SUPPOSED TO LIVE UR LIFE AND U NEED TO LIVE IT WITHIN UR MEANS (UNATAKIWA UISHI MAISHA YAKO NDANI YA UWEZO WAKO)

KAMA HUNA HIYO HELA au hela uliyonayo umeibajeti kufanyia mambo mengine then DON'T SPEND IT. Vijana wengi tunafeli maisha kwa kuwa WE WANT TO SHOW OUR FRIENDS KUWA WE LIVE BEYOND OUR MEANS kumbe kiuhalisia mfukoni hatuna kitu.