SABABU ZA KUTUMBULIWA KWA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI (DCI)

Rais John Pombe Magufuli wikiendi iliyopita, ametoa uamuzi wa kumtungua Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamanda Diwani Athumani Msuya, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi Dar es Salaam jana,  na kuzua sintofahamu kwa watu kujiuliza ni kwanini Mkuu huyo wa upelelezi atumbuliwe?



Ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu ateuliwe mwezi Mei mwaka jana na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa anashika nafasi hiyo,  Bw. Robert Manumba, ambaye alistaafu kwa mujibu wa Sheria.

Vyanzo ndani Serikalini vimesema kwamba, Diwani ametenguliwa na Rais kwa kile kinachosemekana kwamba Diwani alishindwa kuendana na kasi ya kazi anayoitaka Rais na vile vile  Rais hakuridhia na utendaji wake wa kazi sana sana katika kupambana vita dhidi ya wahujumu uchumi, ujangiri na ujambazi wa kutumia silaha kutokana na vita hivyo kuendelea kushamiri huku upande wa Serikali kuonekana kuzidiwa.

Kazi kubwa kabisa ya kitengo hicho ni kufanya uchunguzi au upelelezi wa kutosha zitakazowapa polisi nafasi kubwa ya wao kuwa mbele au sambamba na uhalifu wote unaotokea, na kupelekea kukamatwa kwa vilinge vya majambazi wakubwa lakini hadi sasa kila kitu kinaenda kwa kasi ya konokono, ukizingatia mauaji ya polisi nayo yanaongezeka mfano ni mwezi wa Agosti tu hapo ambapo mapolisi wanne waliouawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

Kazi nyingine ni kuongoza upelelezi wa kwenye makosa makubwa yanayohusiana na udanganyifu, ujangiri na usafirishwaji wa nyara, ujambazi wa kutumia silaha, madawa ya kulevya, utakatishaji wa fedha na makosa ya kuhujumu uchumi. Kazi ya DCI, ni kufanya uchunguzi katika hayo yote na kujitahidi kuyazuia yasitokee na watu wengi wamesema Diwani hakua mtu sahihi kwa kazi hiyo.

#TheGuardian