TAASISI YA DORIS MOLLEL YAPOKEA VITABU 250 KUTOKA KWA KAMPUNI YA MAK SOLUTIONS.



Tarehe 11 mwezi wa kumi wa kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya wasichana duniani. Katika kuelekea siku hiyo, tarehe 9/10/2016 Taasisi ya Doris Mollel chini ya mkurugenzi wake wa Idara ya Elimu Bi. Rahma Amood alipokea vitabu vya kiada 250 kutoka kampuni ya MAK SOLUTIONS.

Kampuni ya MAK SOLUTIONS inayohusika na uuzaji na usambazaji wa vitabu, ilitoa vitabu hivyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo yenye lengo la kusaidia shule zenye uhaba wa vitabu hususani za wasichana zinazopatikana katika mikoa ya Arusha, Pwani, Dar es Salaam na visiwani Zanzibar
Bi. Rahma Amood wakati akiongea na waandishi wa habari alikuwa na haya ya kusema “ vitabu ni muhimu sana kwa mwanafunzi kwa sababu vinaongeza uelewa wa kile kinachofundishwa darasani, sisi kama Taasisi ya Doris Mollel tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya MAK SOLUTIONS kwa kuunga mkono jitihada zetu”.

Wakati wa utoaji wa vitabu hivyo, Mkurugenzi wa MAK SOLUTIONS Bwana MEETAL KIRUBAKARAN alisema “tutaendelea kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kwa sababu wameonesha nia ya kusaidia wasichana ili waweze kupata elimu bora, hivyo basi kwa kupitia wao tutaweza kuwawezesha wasichana wengi katika jamii yetu”.