Tanzania: Wanasayansi wagundua nyayo 400 za binadamu wa kale katika tabaka la ardhi

Wanasayansi na watafiti wamepata ushahidi wa kipekee sana duniani kwa kupata nyayo Zaidi ya 400 za mwanadamu wa kale katika tabaka linalokadiriwa kuwa na miaka 5000 mpaka 19,000. Nyayo hizo ni za makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wametembea juu ya tope la majivu ya volcano pembezoni mwa Ziwa Natron katika site iliyopewa jina la Engare Sero, sio mbali na mlima wa volcano wa Ol Doinyo Lengai (Mlima wa Mungu kwa tafsiri ya Kimasai).



Kuna nyayo nyingine za 3.5 Millioni ambazo zipo Laetoli na zinashikilia rekodi ya kuwa nyayo za kale Zaidi. Pia kuna nyayo za South Afrika ambazo zinakadiriwa kuwa na miaka 117,000 zilizogundulika mwaka 1995.

Nyayo hizi zilizogundulika hivi karibuni zina upekee sana kutokana na wingi wa nyayo na zimehusisha watu wa aina nyingi. Katika vipimo vya foot anatomy inaweza kuonyesha size ya individual, ukubwa wa mwili pamoja na umri. Hii itasaidia pia kuchunguza tabia za jamii. Hii ni kutoka kwa Dr Cynthia Liutkus-Pierce kutoka chou kikuu cha Appalanchian State University ambaye ni geologist na mwanachama wa National Geographic Channel. Kipimo cha umri wa hizo nyayo kilitumia Radiometric dating ya kupima crystals za udongo mgumu wenye hizo nyayo.

Hii ni mojawapo kati ya tafiti kubwa duniani kuhusiana na mambo kale katika bara la Africa hususani Tanzania. Tanzania imekuwa ikiwa na ushahidi na site kubwa zinazofahamika duniani lakini je tunazitumia vipi hizo site katika kuleta maendeleo?