Teknolojia mpya ya gharama nafuu ya ujenzi wa barabara ambapo kwa sasa kilomita moja itajengwa kwa siku moja



Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia gharama kubwa ya kujenga barabara kwa kila kilomita hali ambayo pengine ndio imefanya kwenye baadhi ya maeneo kuendelea kuwa na barabara mbovu, Tanzania kwa sasa imekaribisha Teknolojia mpya ya gharama nafuu ya ujenzi wa barabara ambapo kwa sasa kilomita moja itajengwa kwa siku moja.

Lilian Kimaro ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Divine Connections akiongea kupitia kipindi cha #PowerBreakFast kuelezea kuhusu teknolojia hii iliyobuniwa na wataalam kutoka Israel na Marekani ambapo kwa majaribio yamefanywa kwenye barabara ya Kimara Suka kwenda Golani imejengwa kwa umbali wa robo kilomita.

Lilian Kimaro alisema "Hii teknolojia inamilikiwa na Israel na mvumbuzi wake anaitwa Yosef Atoon ambaye alivumbua technology inaitwa ZYM TEC inayotumia vimeng'enyo maalum viko katika aina ya maji unavichanganya na maji labda ya lita elfu sita unachanganya kwenye barabara kwenye udongo husika ukishachanganya basi unakuwa umemaliza"