Walioiba' wameitikia agizo lake la kuwataka kujisalimisha

kukaguliwa, wameitikia agizo lake la kuwataka kujisalimisha na kufanyika ukaguzi ili kujiridhisha bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo.



Mwishoni mwa wiki, Mwijage alitoa siku nne kwa wafanyabiashara ambao wanadaiwa kutorosha makontena 100 bandarini, wajisalimishe Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili yakaguliwe. Ili kutekeleza agizo hilo waziri huyo aliweka dawati la dharura kutoa huduma hiyo katika siku za mapumziko.

Alisema wafanyabiashara ambao wangekaidi agizo hilo, wangechukuliwa hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kulipa faini ya asilimia 15. Ukaguzi huo ulitakiwa kufanywa na TBS kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC). Lengo la ukaguzi huo ni kubaini bidhaa zilizoingizwa nchini na ubora wake.

Alisema kuna wafanyabiashara wanaleta makontena yana nguo, ambazo zina kiwango cha chini na wengine hawalipi kodi, wengine wanaleta vilainishi vya magari wakati hapa nchini, pia kuna kiwanda cha kuzalisha vilainishi hivyo, hivyo kuruhusu makontena kupita bila kukaguliwa ni kuua viwanda vya ndani. 

#HabariLeo