Wastara Juma alilia Serikali kuhusu kushuka kwa Soko la Filamu za Kibongo Nchini

Katika Miaka ya hivi karibuni Soko la filamu kushuka kwa kiwango kikubwa nchini na moja ya sababu ni uuzwaji holela na ukodishwa wa kazi za wasanii na kudhorotesha tasnia ya filamu. Katika mtandao wa Instagram msanii Wastara Juma ameandika ujumbe unaolenga Serikali kutochukua hatua stahiki kunusuru Soko la Filamu.



Ujumbe wa Wastara
Ukiitazama hizi picha unagundua kuwa filamu ni kitu kikubwa sana.
Leo filamu zinakufa kwa sababu nyingi tu ikiwemo ubora, maharamia, kukosa udhibiti wa filamu za nje, filamu za tafsiri na mengine mengi sana. lakini cha kustaajabu wanasiasa wote wako kimya kuizungumzia tasnia iliyokuwa inatoa ajira kwa takribani Watanzia Laki Tano. Tunalipa kodi nyingi tu kila siku.Withholding Tax kwa  maproducer, 
Stika za TRA, CosotaBodi ya Filamu na Libraly zote zinalipa kodi.


Lakini leo serikali inaruhusu filamu za nje kuuzwa hata bila kulipa kodi. kwakweli inauma sana. Wasanii Hebu Tuamke Tuiambie Serikali Itutazame Sasa na sio kipindi cha Uchaguzi tu