Siku 10 tangu Rais John Pombe Magufuli apongeze kikosi maalum cha kupambana na ujangili kwa kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa maarufu wa ujangili wa tembo nchini anayejulikana kwa jina la 'Mpemba', sasa imefahamika kwamba idadi ya watu waliokamatwa kwenye kesi hiyo imefikia 15.
Akiwa katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, Rais Magufuli alimpongeza Katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudence Milanzi kwa kumkamata "Mpemba" licha ya jitihada hizo kukutana na vikwazo awali.
Jina la Mpemba, ambalo si halisi la mtuhumiwa, lilikuwa likitajwa kwa muda mwingi wa serikali ya awamu ya nne chini ya Jakaya Kikwete kuwa kinara wa ujangili wa kuua tembo nchini.
Akizungumza jijini mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema watuhumiwa hao jumla ya 15 walikamatwa na nyara, bunduki.
#Nipashe