BUNGENI :Serikali imetenga Sh. Billion 59.5 kwa ajili ya kugawa Sh Mil 50 kwa kila Kijiji

BUNGENI, DODOMA: Serikali imetenga Sh. Bilioni 59.5 katika bajeti ya 2016/17, kwa ajili ya kugawa Sh. Milioni 50 kwa kila kijiji.

Aidha kuhusu changamoto ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu serikali imesema kuwa fedha zilizopo zitatumika katika maeneo mengine ya sekta ya elimu na si mikopo pekee.

Pia serikali imebaini watumishi hewa 19,629 ambao kwa mwezi hugharimu Sh. Bilioni 19.7 na mpaka sasa watumishi 1,663 wamechukuliwa hatua kwa kusababisha uwepo wa watumishi hewa.