Alikiba na Diamond |
Baadhi ya wasanii walitoa maoni kuhusu Bifu hilo, King Crazy GK msanii wa muda mrefu alisema Bifu lao liendelee ila lisiwe personal bali Bifu hilo liwe la Kibiashara ili liweze kuwasaidia kutengeneza Pesa zaidi. Diamond amekuwa wa kwanza kukubaliana na Ushauri baada kukubali kufanya tamasha la pamoja ili nani ajulikane ni mkali.
Diamond alipohojiwa jana kwenye Redio ya Clouds Fm katika kipindi cha XXL na Bdozen Alisema "yupo tayari itolewe Beat kila mmoja akaingize Vocal ili tuone nani ni Mkali na akaongezea kuwa yeye atafanya Nyimbo hiyo ndani ya Siku moja"
Vile amesema yupo tayari Kufanya Tamasha la Pamoja ili ajulikane nani Mkali kati yake na Alikiba.
Una Maoni gani ndugu msomaji na Mdau wa Muziki kuhusu maneno ya Diamond????
By Emmanuel Mahundi