KESI ZA MIGOGORO YA NDOA ZAONGOZA KULIKO ZA ARDHI NCHINI

Wizara ya Sheria na Katiba imesema  migogoro ya ndoa ni miongoni mwa mashauri yaliyoshika kasi kwa kuongoza kuripotiwa ukilinganisha na mengine nchini.



Kati ya Januari hadi June mwaka huu mahakama zimepokea kesi 4,982 huku kati ya mashauri 1,282 yanatokana na migogoro ya ndoa, mashauri 1,074 ya kesi za Ardhi, 523 ni matunzo ya watoto, makosa ya jinai yakiwa 148, ukatili wa kijinsia 373 na migogoro  ya kazi 148.

Hayo yamebainishwa na waziri wa Katiba na sheria Dk Herisson  Mwakyembe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muswada wa sheria ya msaada wa kisheria uliowasilishwa bungeni hivi karibuni  ambao utaanza kujadiliwa na umma hivi karibuni

Mwakyembe alisema kuwa migogoro ya ndoa ni tatizo kubwa linaloendelea kukua kwa kasi na kwama limejitokeza katika maeneo mengi nchini.