JANUARY MAKAMBA: FIESTA NI TEMBO MKUBWA KWENYE MUZIKI

JANUARY MAKAMBA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira,  January Yusuph Makamba leo alikuwa katika kipindi cha #Clouds360 ambapo alizungumza mambo mengi kuhusu Mazingira hususan ziara aliyoifanya katika Mikoa 10 wiki chache zilizopita.

Mwishoni mwa Mazungumzo hayo Mh January alizungumza kuhusu #Fiesta2016 " Nasikitika sana kesho sitakuwepo kwa sababu nitakuwa Bungeni Dodoma. Lakini ukizungumzia Fiesta,  unazungumzia Taasisi.  Huwezi kuongelea muziki bila kutaja hili lidude likubwa; huyu TEMBO MKUBWA SANA anayeitwa #Fiesta. 

Mimi naitazama sana katika namna ambavyo inachangia kwenye Uchumi wa Taifa, lakini pia namna ambavyo inatoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao. Najua kina Joseph Kusaga,  Ruge na timu nzima imejipanga vizuri sana kwa Fiesta ya kesho lakini pia lazima wajipange kuipeleka Fiesta juu zaidi kwa sababu Fiesta ikienda juu na muziki wetu unaenda juu zaidi". Mh January pia aliwapongeza Wasanii wa Kitanzania kwa kuongeza ubunifu katika kazi zao.