Ripoti hiyo inaonesha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo kutokana na kukosa pesa. Serikali imeshindwa kupeleka fedha za maendeleo katika miradi hiyo. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita serikali ilitakiwa kutoa TZS Bil.824.4 lakini iliweza kutoa TZS B.387 tu.
Wakati BOT ikitoa taarifa hiyo, leo hoteli ya Tai Five ya jijini Mwanza imepigwa mnada kwa kushindwa kulipa deni lake bank. Huko mkoani Kilimanjaro tunaambiwa shule mbili za sekondari (Shigatini Secondary na Usangi Girls secondary) zitapigwa mnada tar.03/12/2016 kufidia deni la benki wanalodaiwa na benki ya maendeleo ya watu wa Mwanga (MDB).
Hii ina maana walimu wa shule hizo wanapoteza ajira, punde si punde wataingia kwenye loop la "jobless people" na kuanza kusaka ajira mtaani. Wanafunzi nao watapata usumbuf wa kisaikolojia wa kuanza kutafuta shule nyingine za kuhamia.
Wakati hayo yakiendelea kutokea tunaambiwa benki nyingi zimedorora na nyingine zimefilisika.Twiga Bancrop Bank ipo kwenye mdororo mbaya sana kiuchumi, na ina hatari ya kufilisika.
Wakati huohuo mzunguko wa pesa umekua hafifu na biashara nyingi zinajiendesha kwa hasara. Mishahara ya watumishi wa umma imeshindwa kuongezeka mwaka huu kama ilivyo utaratibu wa kupandisha mishahara kila mwaka. Ajira mpya zimesitishwa, posho na marupurupu kwa watumishi wa umma zimefyekwa. Lakini bado mtaani hali ni ngumu.
Je haya yote yanasababishwa na nini? Kwanini mzunguko wa fedha ni mdogo sana mtaani wakati TRA wanajisifu kukusanya zaidi ya target kila mwezi? Kwanini hata bunge linakosa pesa za kujiendesha? Kwanini serikali haina pesa za kupeleka kwenye miradi ya maendeleo while kila mwezi TRA wanavuka malengo ya makusanyo? Kwanini serikali inashindwa hata kununua dawa muhimu hospitalini wakati tunaambiwa makusanyo ni makubwa? Je fedha hizo zinaenda wapi?
Maswali yote hayo yatajibiwa hapa kesho na Mhe.Jesca Kishoa Kafulila, kupitia hoja yake aliyoiwasilisha bungeni tar.03 November mwaka huu. Mhe.Jesca alieleza sababu za yote haya na kutoa ushauri kwa serikali. Kesho nitafanya uchambuzi wa hotuba yake hiyo ya kizalendo inayoeleza kama taifa tulipojikwaa na tufanyeje kusonga mbele.
Watu wengi hawajui kwamba zaidi ya 70% ya pato la taifa kila mwezi kuna mahali linaenda ambako mtanzania wa kawaida hanufaiki nalo kwa vyovyote. Je zinaenda wapi? Kufanya nini? Tukutane hapa kesho asubuhi kuichambua hotuba ya Mhe.Jesca Kishoa na tuibebe kama agenda ya kitaifa kushinikiza serikali kufanya maamuzi kwa maslahi ya nchi.
Malisa GJ
1 comments:
Ni Makala mazuri sana keep it up.... But I think this is copied from Malisa Godlisten page... By the way nothing wrong